JINSI YA KUPIKA KUKU NA NDIZI ZA MSHALE

KUKU NA NDIZI MSHALE NI SAFI SANA KWA MLO KAMILI USIKU AU MCHANA PIA UNAWEZA WEKA KARANGA AU TUI LA NAZI. KARIBU JIFUNZE KUPIKA KWA KUFUATA MAELEKEZO HAPA CHINI Kwa ndugu zangu mliopo ughaibuni ndizi si nzuri san kama ndizi inayotoka Moshi, Arusha au bukoba kwahiyo njia hii ya upishi itakufanya ufurahie sana na usione tofauti ya ladha na kula ndizi laini na safi kabisa Menya ndizi zako kisha zipake mafuta ya kupikia na chumvi kisha ziweke kwenye oven kwa dakika 15 hadi 20 zitakua zimeiva na laini za kutosha Pia kuku ipake kitunguu swaumu, pili pili manga, chumvi kisha iweke kwenye oven bila maji itajipika safi na kutoa mchiz kiasi pia utautumia kwenye pishi lako la ndizi oven inasaidia kupika vizuri bila nyama kurojeka na hupotezi vile viuongo kama huna one basi chemsha katika sufuri kwa moto mdogo bila ya kuweka maji ili maji yatakayojichuja toka kwa kuku yataweza kuivisha nyamachunga yasikauke. Weka kitunguu ...