Nyama ya ng'ombe ya kukaanga yenye utamu wa kipekee

Mahitaji
Nyama  - kilo 1
Mafuta ya kula - 1/2 lita
Chumvi
Ndimu (Limao au vinegar) 1
Tangawizi  - 1
Kitunguu saumu  - 1
Cube magic
Viazi - 6
Viungo vingine upendavyo kwenye sauce*.

Maelekezo
Tayarisha nyama yako - kata, osha.
Weka limao, ndimu au vinegar kwenye nyama, ichanganye ili limao lichanganyike vizuri.
Ponda tangawizi kwenye kinu, iwe laini.
Ponda kitunguu swaumu kwenye kinu, ilainike vizuri.
Weka viungo - chumvi, cube maggie, tangawizi na kitunguu saumu kwenye nyama. Changanya nyama ili viungo vipate kuchanganyika vizuri. Acha nyama ikae kwa dakika 40 kwenye jokofu ili viungo viingie vizuri. Jinsi viungo vinavyokaa vizuri kwenye nyama ndio inazidi kunoga.
Bandika sufuria au kikaangio jikoni, weka mafuta kiasi. Subiria yapate moto.
Weka nyama kwenye mafuta.  Koroga ili ichanganyike vizuri na mafuta kisha funika sufuria au chungu na mfuniko. Fanya hivi ili kuiacha nyama ikaangwe na mafuta lakini inaiva na mvuke wake pia.
Geuza geuza nyama kila mara ili kuzuia isigande kwenye chombo cha kupikia. Subiria hadi iive.
Angalia kama nyama imeiva. Unaweza kuongeza pilipili manga ya unga ili kuleta ladha tofauti kwenye nyama.
Ukimaliza unaweza kutenga na kula. Ni vizuri ukala kwa kachumbari nzuri pamoja na kinywaji upendacho.


Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUPIKA KUKU NA NDIZI ZA MSHALE

JIFUNZE KUTENGENEZA CAKE