JINSI YA KUPIKA KUKU NA NDIZI ZA MSHALE
KUKU NA NDIZI MSHALE NI SAFI SANA KWA MLO KAMILI USIKU AU MCHANA PIA
UNAWEZA WEKA KARANGA AU TUI LA NAZI.
KARIBU JIFUNZE KUPIKA KWA KUFUATA MAELEKEZO HAPA CHINI
Kwa
ndugu zangu mliopo ughaibuni ndizi si nzuri san kama ndizi inayotoka
Moshi, Arusha au bukoba kwahiyo njia hii ya upishi itakufanya ufurahie
sana na usione tofauti ya ladha na kula ndizi laini na safi kabisa
Menya
ndizi zako kisha zipake mafuta ya kupikia na chumvi kisha ziweke kwenye
oven kwa dakika 15 hadi 20 zitakua zimeiva na laini za kutosha
Pia
kuku ipake kitunguu swaumu, pili pili manga, chumvi kisha iweke kwenye
oven bila maji itajipika safi na kutoa mchiz kiasi pia utautumia kwenye
pishi lako la ndizi oven inasaidia kupika vizuri bila nyama kurojeka na
hupotezi vile viuongo kama huna one basi chemsha katika sufuri kwa moto
mdogo bila ya kuweka maji ili maji yatakayojichuja toka kwa kuku
yataweza kuivisha nyamachunga yasikauke.
Weka
kitunguu maji kwenye sufuria yenye mafuta moto kisha weka binzali
koroga kwa dakika moja kisha weka nyanya ya kopo koroga kiasi kisha weka
kuku na ule mchuzi wake kwenye sufuria kisha mimina zile ndizi acha
ichemke kwa dakika 5 hadi 7 ndizi yako itakua safi na imelainika kabisa
utafurahia chakula kitamu na rahisi kupika usisahau kuweka chumvi.
Muonekano wa ndizi na kuku ndani ya sufuri zikichemka
Hiki ndio chakula kimeshaiva unaweza kula na salad mchanganyiko au parachichi ohhhh safi sana siku inapita ukiwa na furaha.
wooooooh the food is so delicious .
imeandaliwa na ARTTU KONZO..........miss delicious
Comments
Post a Comment