JIFUNZE KUTENGENEZA CAKE

Mapishi ya keki

Siku zote mtu anatakiwa awe mbunifu kwa kila kitu.Ila leo nagusia upande wa jikoni.Kwa upande wa wanawake katika sekta nzima ya maakuli mambo ya jikoni shuti unatakiwa uwe mtundu,leo unabuni hiki na kesho unafanya vile ili mradi uweze kupata vionyo tofauti tofauti.Raha ya chakula shuti upike mwenyewe bibi..'mwanamke jiko eeh''.
Leo tutaangalia namna ya kupika keki ya kawaida hasa ukiwa nyumbani.Karibuni tujifunze pamoja
Mahitaji:
Unga wa ngano glasi 4
Mayai 10
Sukari glasi 3
Baking powder vijiko 2 vya chai
Unga wa mdalasini kijiko 1 cha chai
Zabibu kavu
Maziwa fresh 1/2 glasi na mtindi 1/2 glasi
Cocoa au kahawa
Vanila
tui la nazi zito kabisa,kiasi
Mafuta 1/4 lt
Tray ya kuokea keki yako
Sufuria/chombo cha kuchanganyia mchanganyiko wako
Hatua za kupika:
Tayarisha oven yako kwa kuiwasha katika moto wa nyuzi 185 sentigrade (365F)
Paka mafuta kiasi kwenye kikaangio/tray yako kisha kiweke pembeni
Pasua mayai yako kisha yaweke tkt 'brenda',weka sukari yako kisha washa mashine yako ili vichanganyike kwa pamoja hadi viwe laini kabisa.
Weka unga wako ktk sefuria ,weka baking powder,zabibu,mdalasini,cocoa au unga wa kahawa,tui la nazi,maziwa fresh,mtindi,mafuta,vanilla,vichanganye alafu mwisho mimina mchanganyiko wako wa mayai na sukari kisha vichanganye vyote kwa pamoja hadi mchanganyiko wako uwe laini kabisa yaani uwe saizi ya kumiminika km uji.
Chukua mchanganyiko wako huo alafu uumimine ktkt tray yako uliyoipakaa mafuta, ulioiandaa kwa ajili ya kuokea keki yako.
Kisha uweke ktk oven kwa muda wa dk 40-45 kupika keki yako.
Tumia toothpick au kijiti cha mbao kisafi kuchomeka katikati ya keki yako kuangalia kama imeiva vyema, baada ya hizo dakika hapo juu kupita
Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka bila ya ungaunga basi keki yako imeiva vyema, iepue na uzime jiko
Iwapo kijiti cha mbao/ toothpick kitatoka na unga unga basi ujue bado keki yako haijaiva vyema. Funga mlango na uache iive kwa muda. Hakikisha kijiti kinatoka bila ya unga unga
Iache keki yako ipoe kwa dakika 15 - 20 kabla hujaiondoa kwenye kikaangio
Keki yako ipo tayari kwa kuliwa
Waweza kula na soda, chai, juice, maji, maziwa au hata peke yake.
Imeandaliwa na Arttu Konzo,,,,

Comments

Popular posts from this blog

Nyama ya ng'ombe ya kukaanga yenye utamu wa kipekee

JINSI YA KUPIKA KUKU NA NDIZI ZA MSHALE